Friday, October 2, 2015

Introducing TEACHERS UNITED SPORTS CLUB



Teachers` United Sports Club (TUSC) was established in 2012 and  registered in the United Republic of Tanzania in 2014 under the National Sports Council Act of 1967 as amended in 1971 with registration number NSC 10976.Its headquater is located at Mkuranga town in Coast Region.

Our Contact

TEACHERS` UNITED SPORTS CLUB
 PO Box  10
MKURANGA.
Mob:0687800681
 https://www.facebook.com/teacherssc1



Monday, September 9, 2013

UDANGANYIFU WA UMRI WACHEFUA COPA COCA COLA TAIFA.




Timu ya copa coca cola mkoa wa Kinondoni
Mashindano ya copa coca cola taifa ngazi ya kanda yamemalizika katika viwanja mbali mbali wiki iliyopita huku mikoa mingi ikiwa inawakilishwa na vijana wenye umri mkubwa tofauti na matarajio ya wengi kuwa itashirikisha vijana wenye umri wa chini ya miaka kumi na tano tu kama inavyotakiwa. Ukiukwaji huo wa kanuni inayohusu umri umezigharimu timu za miko yote iliyopeleka vija wenye umri unaotakiwa kwa kuwa vijana wao wameshindwa kuonyesha viwango na kufuzu katika ngazi ya fainali kwa kuwa wamekuwa wakicheza na vijana wa umri usiolingana nao.
Timu ya Mkoa wa Pwani iliyocheza na kinondoni
Katika moja ya mechi ambazo mwandishi wetu ameshuhudia timu ya mkoa wa kisoka wa Kinondoni ikichezesha vijana walio kidato cha nne ambao kimantiki hawastahili kuwemo katika mashindano hayo kwa kuwa umri unakuwa umemtupa mkono kustahili sifa ya kushiriki.
Golkipa wa kinondoni inaesemekana yupo kidato cha nne
MFA kama mdau wa soka hapa nchini ambaye pia iliwakilishwa na vijana saba kutoka katika kituo cha kukuza na kuendeleza soka hapa wilayani cha VIKINDU SOCCER ACADEMY inawaomba wale wote wanaohusika katika usaili na maandalizi ya timu kwa ajili ya mashindano hayo kuzingatia umri stahili ili kuleta ushindani wa kweli katika mashindano hayo kwa kuwa kwa kufanya hivyo tutaweza kutoa fulsa kwa wale ambao hawajapata kuonekana kuonyesha uwezo wao.
Mchezaji huyu wa kinondoni anayechezea pia vila squard ya Dar.

Mwanazuoni ADAM FOYA atembelea Vikindu soccer Academy.




Bwana Adam Foya kushoto akizungumza na Raisi wa VSA 

Mwanazuoni Foya Adamu ambaye pia ni mwalimu katika chuo kikuu cha SEKUCO kilichopo Lushoto Tanga wiki iliyopita alipata fulsa ya kukitembelea kituo pekee cha kukuza na kuendeleza mpira wa miguu hapa wilayani mkuranga cha Vikindu soccer academy. Kwa mujibu wa mratibu wa kituo hicho Bwana John Malata , ndugu Foya alitembelea kituo hicho ili kujionea kwa lengo la kujifunza mambo mbali mbali yahusuyo kituo hicho. Mwanazuoni huyo alipata fulsa ya kuonana na Rais wa kituo hicho ndugu Nicholas Kampa  ofisini Jesus Town,mkabala na kanisa katoriki parokia ya Vikindu na kuzungumza kwa kirefu kuhusu mipango mbalimbali ya kituo na kile kilichofanyika hadi sasa.
Bwana Foya akulia akizungumza na mratibu wa kituo Mr. Malata
Aidha bwana Foya alipata fulsa  ya kuonana na baadhi ya vijana katika kituo hicho katika uwanja wa shule ya msingi Kisemvule mahali ambapo VSA wanapatumia kwa muda wakati mchakato wa ujenzi wa uwanja na majengo ya kituo ukikamilishwa. Aidha bwana Foya pia alipata fulsa ya kuonanana kuzungumza na baadhi ya vijana wa kituo hicho waliokuwa wakiendelea na mafunzo yao chini ya mwalimu Miraji Juma katika uwanja wa shule ya msingi Kisemvule. 

Adam Foya mwenye shati jeusi katikati akiwa na baadhi ya wachezaji wa VSA .
Kituo hicho kinatumia uwanja huo kwa muda wakati utaratibu wa ujenzi wa majengo na uwaja kwa ajili ya kituo ukiendelea. Kituo kicho tayari kina eneo la ekari kumi ndani ya kijiji hicho kilichopo katika kata ya vikindu kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa kituo.
MFA inawakaribisha wadau wengine wote kukitembelea kituo hicho na kukisaidia kwa hali na mali ili kiweze kufikia malengo yake ya kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji hapa wilayani Mkuranga na taifa kwa ujumla.

Sunday, August 11, 2013

Introducing Vikindu Soccer Academy



Mr. Nicholas J. Kampa;The VSA`s President
Vikindu Soccer Academy (VSA) is a centre of excellence for young talented players which gives the young players the opportunity to learn and develop their football ability and skills to the highest level as well as enjoying the game and gaining self confidence.


It was registered in the United Republic of Tanzania under the National Sports Council Act of 1967 as amended in 1971 with registration number NSC 10323. The headquarter of Vikindu Soccer Academy is located at Vikindu ward, Mkuranga district in Coast Region.

  
Mr. John J. Malata; The VSA`s Secretary General
 
 
 


The VSA`s  Mission  is “To offer an innovative programs which fosters the development of football industry in the country.”  Where by the VSA`s Goal  is “To be a strong and vital organ that contributes significantly to the growth of football industry in Tanzania.”

The philosophy behind the establishment of the academy is the development o the QUALITY FOOTBALL PLAYERS through two key pillars; EDUCATION & TRAINING

For more infomation about the academy do not hasetate to write to them through the following contact;

Secretary General
Vikindu Soccer Academy
PO BOX 83
Mkuranga-TANZANIA
Email: academy_vikindu@yahoo.com
 
 
 

Sunday, May 12, 2013

Big Stone FC yaibamiza Mkuranga African Sports 2-1















Kikosi cha timu ya Mkuranga African Sports wakipozi kwa picha kabla ya pamabano
  
Habari na Issa Dege,

Timu ya Big Stone FC ya Mkmba Mkerezange imeibamiza timu ya Mkuranga African Sports 2-1 katika mtanange wa ligi daraja la nne hatua kumi na tano bora katika mchezo uliofanyika katika kiwanja cha shule ya msingi Mkuranga jumapili ya leo.
                                  

   












 Kikosi cha Big Stone FC

Katika mtanange huo wafungaji kwa upande wa Big Stone FC walikuwa ni Ramadhan Mcho na Juma Kulenga , huku kwa upande wa goli moja la kufutia machozi la Mkuranga African Sports likipachikwa kimiani na Kassim Mbupu.




Wachezaji wa timu zote mbili wakiendelea na 
mchezo huo



 





 






Washabiki wa timu ya Big Stone FC wakishangilia mara baada ya timu yao kuibuka na ushindi.