Monday, September 9, 2013

Mwanazuoni ADAM FOYA atembelea Vikindu soccer Academy.




Bwana Adam Foya kushoto akizungumza na Raisi wa VSA 

Mwanazuoni Foya Adamu ambaye pia ni mwalimu katika chuo kikuu cha SEKUCO kilichopo Lushoto Tanga wiki iliyopita alipata fulsa ya kukitembelea kituo pekee cha kukuza na kuendeleza mpira wa miguu hapa wilayani mkuranga cha Vikindu soccer academy. Kwa mujibu wa mratibu wa kituo hicho Bwana John Malata , ndugu Foya alitembelea kituo hicho ili kujionea kwa lengo la kujifunza mambo mbali mbali yahusuyo kituo hicho. Mwanazuoni huyo alipata fulsa ya kuonana na Rais wa kituo hicho ndugu Nicholas Kampa  ofisini Jesus Town,mkabala na kanisa katoriki parokia ya Vikindu na kuzungumza kwa kirefu kuhusu mipango mbalimbali ya kituo na kile kilichofanyika hadi sasa.
Bwana Foya akulia akizungumza na mratibu wa kituo Mr. Malata
Aidha bwana Foya alipata fulsa  ya kuonana na baadhi ya vijana katika kituo hicho katika uwanja wa shule ya msingi Kisemvule mahali ambapo VSA wanapatumia kwa muda wakati mchakato wa ujenzi wa uwanja na majengo ya kituo ukikamilishwa. Aidha bwana Foya pia alipata fulsa ya kuonanana kuzungumza na baadhi ya vijana wa kituo hicho waliokuwa wakiendelea na mafunzo yao chini ya mwalimu Miraji Juma katika uwanja wa shule ya msingi Kisemvule. 

Adam Foya mwenye shati jeusi katikati akiwa na baadhi ya wachezaji wa VSA .
Kituo hicho kinatumia uwanja huo kwa muda wakati utaratibu wa ujenzi wa majengo na uwaja kwa ajili ya kituo ukiendelea. Kituo kicho tayari kina eneo la ekari kumi ndani ya kijiji hicho kilichopo katika kata ya vikindu kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa kisasa wa kituo.
MFA inawakaribisha wadau wengine wote kukitembelea kituo hicho na kukisaidia kwa hali na mali ili kiweze kufikia malengo yake ya kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji hapa wilayani Mkuranga na taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment