| Timu ya copa coca cola mkoa wa Kinondoni |
Mashindano
ya copa coca cola taifa ngazi ya kanda yamemalizika katika viwanja mbali mbali
wiki iliyopita huku mikoa mingi ikiwa inawakilishwa na vijana wenye umri mkubwa
tofauti na matarajio ya wengi kuwa itashirikisha vijana wenye umri wa chini ya
miaka kumi na tano tu kama inavyotakiwa. Ukiukwaji huo wa kanuni inayohusu umri
umezigharimu timu za miko yote iliyopeleka vija wenye umri unaotakiwa kwa kuwa
vijana wao wameshindwa kuonyesha viwango na kufuzu katika ngazi ya fainali kwa
kuwa wamekuwa wakicheza na vijana wa umri usiolingana nao.
Katika moja ya mechi
ambazo mwandishi wetu ameshuhudia timu ya mkoa wa kisoka wa Kinondoni
ikichezesha vijana walio kidato cha nne ambao kimantiki hawastahili kuwemo
katika mashindano hayo kwa kuwa umri unakuwa umemtupa mkono kustahili sifa ya
kushiriki.
MFA kama mdau wa soka hapa nchini ambaye pia iliwakilishwa na vijana
saba kutoka katika kituo cha kukuza na kuendeleza soka hapa wilayani cha
VIKINDU SOCCER ACADEMY inawaomba wale wote wanaohusika katika usaili na
maandalizi ya timu kwa ajili ya mashindano hayo kuzingatia umri stahili ili
kuleta ushindani wa kweli katika mashindano hayo kwa kuwa kwa kufanya hivyo
tutaweza kutoa fulsa kwa wale ambao hawajapata kuonekana kuonyesha uwezo wao.
| Timu ya Mkoa wa Pwani iliyocheza na kinondoni |
| Golkipa wa kinondoni inaesemekana yupo kidato cha nne |
| Mchezaji huyu wa kinondoni anayechezea pia vila squard ya Dar. |
No comments:
Post a Comment