Klabu ya Vikindu warriors fc ya Vikindu imeendelea kusua sua katika mashindano ya ligi daraja la tatu mkoa wa Pwani. Ligi hiyo ambayo kwa sasa imesimama kupisha dirisha dogo la usajili baada ya mzunguko wa kwanza kumalizika inatarajiwa kuanza tena katikati ya mwezi wa kwanza 2013.
Katika kundi linalohusisha klabu mbili za Mkuranga,Black tiger na Vikindu, Black tiger inaongoza kundi hilo ikifuatiwa na Wagadugu ya Mafia wakati Ikwiriri united ya Ikwiriri Rufiji na Al-Ithadi ya Mafia zinashika nafasi ya tatu na nne.

No comments:
Post a Comment