Sunday, December 30, 2012

LIGI DARAJA LA NNE: EGON FC YAICHAKAZA BIGSTONE FC 4-2


Kikosi cha EGON FC
 Ligi daraja la nne wilaya ya mkuranga imeendelea teana leo katika uwanja wa shule ya msingi Kimanzicha ambapo timu za Bigstone ya  Mkerezange na Egon Fc ya Kilimahewa zimemenyana. Mchezo huo ulioshuhudiwa na umati mkubwa wa watu ulimalizika kwa kushuhudia Egon Fc ya Kilimahewa a.k.a watoto wa paroko wakiibuka na ushindi mnono wa magoli 4 kwa 2 mbele ya Bigstone fc.Wafungaji wa magoli hayo kwa upande wa Egon FC ni Cosmas Victory Laisi aliyefunga magori matatu [3] na Samwel Mapunda goli moja [1] wakati kwa upande wa Bigstone wafungaji ni Ally Kulonga na Moshi Sultan

Bigstone Fc
Mwamuzi wa kati  wa mchezo huo alikuwa ni Sabuki S. Sabuki akisaidiwa na Christopher James na Twahili Mamboya.

Katika mwendelezo wa ligi hiyo, taarifa za mechi zilizochezwa jana tarehe 29/12/2012 ni kama ifuatavyo:
Katika uwanja wa shule ya msingi Vianzi Yosso FC ili wakaribisha SalimFC ya Mwanambaya na matokeo ni sare ya 1:1; Katika uwanja wa shule ya msing Mkuranga Mkuranga African waliikaribisha Bombwe FC na Mkuranga African waliibuka na ushindi wa magoli 2 kwa bila; Katika uwanja wa shule ya msingi Kimanzichana Barcelona Fc iliikaribisha New Generatin FC na Barcelona walishinda 1:0 ; Katika kiwanja cha Shungubweni Small stone fc iliwakaribisha Rangers fc ya Kisayani na matokeo timu zote zilipishana nguvu kwa kufungana magoli 3:3.

Waamuzi wa mechi kati ya Egon fc ya kilimahewa na Bigstone fc ya Mkerezange.


No comments:

Post a Comment