Friday, February 15, 2013

MATUKIO KATIKA PICHA

Ukata waitoa Vikindu Warriors ligi daraja 3 mkoa


Golkipa wa zamani wa sima,coast union na banadri mtwara,
Miraji juma amabye pia ni kocha wa timu ya Vikindu Warriors FC
akitoa maelekezo ya mwisho kabla ya mechi kati yao na
 Black Tiger Fc katika uwanja wa Mwanambaya Complex.
  Timu ya Vikindu Warriors fc inayoshiriki ligi daraja la 3 mkoa wa Pwani imejiondoa rasmi katika ushiriki wa ligi hiyo kutokana na ukata mkubwa unayoikabili timu hiyo.

Mmoja wa wadau wakubwa wa timu hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alithibitisha kuwa tayari uongozi wa klabu hiyo umekiandikia chama cha mpira wa miguu mkoa wa Pwani [COREFA] kwa ajili ya kujiondoa katika ligi.

Timu hiyo ilishindwa kwenda mafia kucheza mechi zake mbili na klabu za Al-itihad na Wagadugu Fc mwishoni mwa mwezi uliopita.

Wadau wa soka wilayani hapa wameelezea kusikitishwa kwao na hali iliyojitokeza kutoka na wilaya hiyo kubakiwa na timu moja tu ya Black Tiger katika ligi hiyo inayoendelea kutokana na timu nyingine ya Binga Stars kushindwa kushiriki kwa sababu za ukosefu wa fedha kama ilivyo kwa vikindu.