Sunday, May 12, 2013

Big Stone FC yaibamiza Mkuranga African Sports 2-1















Kikosi cha timu ya Mkuranga African Sports wakipozi kwa picha kabla ya pamabano
  
Habari na Issa Dege,

Timu ya Big Stone FC ya Mkmba Mkerezange imeibamiza timu ya Mkuranga African Sports 2-1 katika mtanange wa ligi daraja la nne hatua kumi na tano bora katika mchezo uliofanyika katika kiwanja cha shule ya msingi Mkuranga jumapili ya leo.
                                  

   












 Kikosi cha Big Stone FC

Katika mtanange huo wafungaji kwa upande wa Big Stone FC walikuwa ni Ramadhan Mcho na Juma Kulenga , huku kwa upande wa goli moja la kufutia machozi la Mkuranga African Sports likipachikwa kimiani na Kassim Mbupu.




Wachezaji wa timu zote mbili wakiendelea na 
mchezo huo



 





 






Washabiki wa timu ya Big Stone FC wakishangilia mara baada ya timu yao kuibuka na ushindi.